WATENDAJI SONGWE WAPIGWA MARUFUKU KUTOA VIBALII KWA WAFUGAJI KIHOLELA
Chongolo ameagiza watendaji wa vijiji na kata kuacha mara moja kuingiza kiholela wafungaji pamoja na mifugo yao katika vijiji vyote mkoani Songwe na kutaka ofisi za wakuu wa wilaya ndio ziwe zinatoa vibari hivyo kwa kushirikiana na ofisi wa wakurugenzi wa halmashauri za mkoani Songwe.
Chongolo ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua miradi na kujitambulisha kwa wananchi wa wilaya Momba ambapo amedai kumekuwepo na migogoro inayoweza kuepukika lakini kutokana na utoaji holela wa vibari hivyo ndio sababu ya migogoro mingi ya wakulima na wafugaji kutoa.
"Kijiji kinaruhusu uingiaji wa mifugo kiholela na hakuna eneo la malisho unategea nini kama sio kuleta migogoro ya wakulima na wafugaji? Kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji au kiongozi yoyote wa Kijiji kutoa kibari cha mifugo natoa agizo ofisi za wakuu wa Wilaya ndio zitatoa vibari hivi kwa kushirikiana na Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri" alisema Chongolo
Aidha Chongolo amesema kuna kila dalili za rushwa katika utoaji wa vibari hivyo na mwisho wake ndio kutoa vibari kwa njia zisizo salama.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Songwe amesema kuanzia sasa kibari za kuuza ardhi kitatolewa na maafisa tarafa na sio viongozi wa kijiji na ametoa onyo kwa watendaji wa vijiji kutothubutu kutoa vibari na kwa kipindi hiki alichopewa Mkoa wa Songwe atahakisha hili analisimamia

Maoni