WATU 18 WAJERUHIWA BASI LA TAKBIIR LAPINDUKA SINGIDA
WATU 18 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Takbiir lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Katoro mkoani Geita kupinduka.
Basi hilo lenye namba za usajili T 278 DTZ limepinduka saa 1: 00 asubuhi leo Mei 23, 2024 katika eneo la Manga nje kidogo na Manispaa ya Singida.
Majeruhi wa ajali hiyo wakizungumza na Nipashe Digital ambayo ilifika muda mfupi baada ya ajali kutokea wamesema basi hilo lilipunduka baada ya kutaka kulipita gari dogo na kugonga daraja dogo na kupinduka.

Nipashe Digital ambayo imefika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea imeshuhudia majeruhi wakichukuliwa na magari ya wagonjwa (ambulance) wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mandewa mkoani Singida.
Maoni