BILIONI 2 KUJENGA CHUO CHA AFYA VWAWA,MBOZI
SERIKALI imetenga Sh bilioni 2.9 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Afya Vwawa mkoani Songwe.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ujenzi wa chuo hicho utaanza Oktoba 2024.
Waziri Ummy ametoa taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga aliyetaka kujua lini Serikali itajenga chuo cha afya Vwawa.
Aidha, Waziri Ummy amesema tayari utaratibu wa kupata eneo umefanyika ambapo shilingi Milioni 151 zimetumika kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliopisha eneo hilo.
Amesema chuo hicho kitakua kinatoa mafunzo kwa ngazi ya astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) kwa kozi za uuguzi pamoja na nyingine ambazo ni muhimu katika utoaji wa huduma za afya ikiwemo wataalam wa maabara.

Comments