MBUNGE SICHALWE: TUWEKEWE GETI MPAKA WA MOMBA-ZAMBIA, TUONGEZE VYANZO VYA MAPATO



Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe Condester Sichalwe (Mundy) akiwa Bungeni Jijini Dodoma kwa mara nyingine ameiomba Serikali kufanya juu chini kufungua geti la pili katika mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la kijiji cha Chipumpu Halmashauri ya Momba ili kupunguza mianya ya uigizwaji na utoroshaji wa bidhaa mbalimbali kupitia maeneo hayo na kuikosesha Serikali Mapato.


Mhe. Sichalwe amesema tangu mwaka 2021 amekuwa akisimama mara kdhaa Bungeni hapo na kutoa wazo la kuongeza geti eneo hilo, badala ya kutegemea mpaka wa Tunduma Pekee kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza vyanzo vya mapato na kupunguza mianya ya uingizwaji na utoroshaji wa bidhaa kinyemela.


“Swali langu ni kwamba je nilini Serikali itaboresha mpaka kati ya Zambia na Tanzania ili kudhibiti njia za panya ambazo mazao na bidhaa nyingine hutoroshwa bila kulipiwa kodi” Mhe.Sichalwe


Naibu waziri wa Fedha Mhe.Hamad Hassan Chande akijibu swali hilo amesema kuwa katika kudhibiti utoroshaji wa bidhaa na mazao katika mpaka wa Tanzania na Zambia, Mamlaka ya mapato Tanzania TRA na Mamalaka ya mapato ya Zambia ZRA wameingia makubaliano ya pamoja ya kubadilishana taarifa ili kudhitibi hali hiyo.


Mhe. Chande amesema hata hivyo TRA imendelea kuhimalisha dolia katika maeneo yote ya mpaka wa Tanzania na Zambia isiyo rasmi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kulinda mapato ya nchi.


Kuhusu hoja ya Mbunge wa Momba ya kujengwa kwa Mageti mengine ya Chipumpu, Kapele na Kalambo Naibu Waziri Chande amesema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kujilidhisha zaidi na maeneo hayo na kama yataonekana yanatija ya kuongezwa kwa mageti Serikali itafanya hivyo kwa kushirikiana na Serikali ya Zambia.


Mwaka 2022 waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alifika Jimbo la Momba kwa mwaliko maalumu wa Mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya kutembelea eneo ambalo linalopendekezwa kujenga geti hilo kijiji cha Chipumpu kata ya Kapele na kusema kuwa Serikali inachukua wazo la Mbunge Sichalwe kwa ajili ya kulifanyia kazi.


Kiu na Matamanio ya Mbunge wa Jimbo la Momba ni kuona Serikali haipotezi mapato kwa kuongeza vyanzo vya mapato kupitia mpaka huo, kwani hivi sasa kuna njia nyingi za panya ambazo zinatumika kimagendo kuzuvusha na kuingiza bidhaa kinyemela bila kulipiwa kodi.


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE