KENYATTA ATAKA WAANDAMANAJI WASIKILIZWE


 NAIROBI, Kenya - Rais wa zamani Kenya, Uhuru Kenyatta ameeleza kusikitishwa kwake juu ya hali ya taifa hilo linalokumbwa na maandamano dhidi ya Mswada wa Fedha akisisitiza kuwa ni haki ya wakenya kuandamana.


Mkuu huyo wa zamani wa Nchi alituma rambirambi zake kwa Wakenya waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya Jumanne akisema ni haki yao ya kikatiba na wanapaswa kusikilizwa na walioko madarakani.

"Ninakuja kwenu nikiwa na huzuni kubwa kutokana na hali ya sasa nchini. Ni haki ya Wakenya kuandamana kama ilivyoamuliwa na Katiba ya Kenya ya mwaka 2010. Pia ni wajibu wa viongozi wasikilize wanaowaongoza," amesema Uhuru.

Aidha Uhuru ametoa wito wa utulivu na kuwataka viongozi kuzungumza na wananchi.

"Kama rais wenu wa zamani nimehisi uzito wa kuwaongoza Wakenya. Kwa hivyo naomba hekima na ustaarabu uimarishwe na amani na maendeleo yawe yetu sote kama watoto wa Kenya," alisema.

Rais huyo wa zamani alithibitisha uungaji mkono wake kwa Wakenya na kuwataka viongozi "Wazungumze na watu."

"Naomba amani na uelewano kwa kila Mkenya na sisi sote tukumbuke kuwa Kenya ni kubwa kuliko mmoja wetu; hakuna kitu kilichopigwa mawe ambacho hakiwezi kubadilishwa,"

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE