POLISI YAWATAHADHALISHA BOBA BOBA NA BAJAJ DHIDI YA WANAFUNZI WA KIKE
Madereva wa Bajaji na Pikipiki maarufu Bodaboda Mkoa wa Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwafanyia vitendo vya ukatili wanafunzi wa kike pindi wanapokwenda na wanaporudi shuleni ili wanafunzi waweze kutimiza malengo yao ya baadae.
Wito huo ulitolewa Juni 26,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji Jamii kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma Naibu kamishna wa Polisi (DCP) Herry Mwaibambe wakati akitoa elimu kwa madereva bajaji katika ukumbi wa Polisi uliopo Vwawa Wilaya ya Mbozi na kuwataka madereva hao kutoa taarifa za uhalifu na ukatili wa kijinsia kwa Jeshi la Polisi pindi waonapo mtoto au mwanafunzi anafanyiwa vitendo hivyo ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka ikiwa ni pamoja na watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.
Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi SACP Martini Otieno kutoka Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo amewaeleza madereva hao umuhimu wa kuwa na leseni ikiwa ni pamoja na kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kushiriki kikamilifu bila kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi
Comments