RC APONGEZA UTENDAJI KAZI WA DED BIEDA KIBAHA

 


MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema hati safi kwa Mkoa huo imekuwa jambo la kawaida na kwasasa Mkoa huo unakwenda kujikita kwenye matumizi yenye tija.

Kunenge ameyasema hayo June 25 aliposhiriki katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kujadili hoja za Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali.

Amesema kinachoenda kutatua kero za wananchi ni fedha na sio asilimia, na hivyo Mkoa huo kwa sasa umelenga kutengeneza, kukusanya na kuwa na matumizi yenye tija ya mapato.

Kunenge pia amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Regina Bieda kwa namna anavyofanya kazi zake kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ilivyopangwa katika eneo lake.

Naye Katibu Tawala mkoa wa Pwani Rashid Mchatta amepongeza utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo hususani katika kusimamia makusanyo ya mapato.

Mchatta amewataka Watendaji kuhakikisha wanampa ushirikiano Mkurugenzi huyo Ili kufikia malengo ya Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Makala alimuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa wamejipanga vizuri katika ukusanyaji wa mapato na utatuzi wa kero za wananchi.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Regina Bieda alisema Halmashauri hiyo kwa mwaka 2022/2023 hoja zilikuwa 49 kati ya hizo 23 zimefungwa na zilizobaki zinaendelea kufanyiwa kazi hususani kwa zile zilizopo ndani ya uwezo wao.

Bieda pia ameahidi kuzingatia ushauri na maelekezo wanayopewa na kuepuka kuzalisha hoja mpya katika Halmashauri hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE