IMANI ZA KISHIRIKINA NI CHANZO KIKUBWA CHA UKATILI KATIKA JAMII


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amesema imani za kishirikina zinachangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa ukatili uliokithiri katika jamii hivyo ameitaka jamii kuepukana na imani hizo kwani zinapelekea migogoro katika jamii pamoja na mauaji.


Ameyasema hayo Julai 14, 2024 alipokuwa akiongea na waumini wa Kanisa la Efatha lililopo Kisasa Jijini Dodoma na kuwaeleza kuwa tumtegemee mwenyezi Mungu katika kila kitu na kuachana na tamaa ya Mali inayopelekea kwenda katika imani za kishirikina na matokeo yake ni mauaji.

Kamanda Mallya amesema kitu kingine kinachopelekea kuwepo na ukatili uliokithiri ni ulevi uliopitiliza na wivu wa mapenzi ambao hupelekea vipigo na matusi jambo ambalo husababisha ukatili wa kijinsia, ubakaji, kulawiti, kujeruhi pamoja na mauaji.


Katika hatua nyingine Mamanda Mallya amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kubaini changamoto za ukatili wanazokumbana nazo ikiwemo ukatili wa kijinsia, ubakaji na kulawiti huku akisema "mzazi ongea na mwanao" ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kwani wimbi la ushoga na usagaji pamoja na ubakaji limekuwa kubwa.

Aidha Kamanda Mallya amekemea masuala ya rushwa kwa kusema msipokee wala kutoa rushwa kwani hubadili ukweli kuwa uongo na hudhurumu haki ya mtu huku akinukuu vifungu vya biblia katika kitabu cha Kutoka 53:28, Kumbukumbu la Torati 110:17 na Zaburi 15:5 huku akitoa mfano kwa Samsoni alivyosalitiwa na Delilah pia Yuda Eskarioti alipomsaliti Yesu sababu ya rushwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE