KINDAMBA AWATAKA WAGANGA WAFAWIDHI VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI ILEJE KUKUMBUKA WAJIBU WAO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bi. Nuru Waziri Kindamba mapema leo Julai 29,2024 ameongea na Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati zilizopo wilayani hapa ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha juu ya uwajibikaji pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Bi. Kindamba ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo maalumu ya mifumo mbalimbali ya utendaji kazi za Serikali kwa Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati wilayani hapa.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Kindamba amesisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa vifaa sambamba na kuzingatia maslahi ya watumishi wenza pamoja na wateja (wagonjwa) wanaopatiwa huduma.
Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea uwezo Waganga Wafawidhi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kama ilivyo miongozo ya Serikali, miongoni mwa mifumo waliyojifunza ni pamoja na Gothomis na Nest ambayo yote inatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali
Comments