MKUU WA MKOA WA RUVUMA KANALI AHMED ABBAS AMEIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO KWA KUPATA HATI SAFI
Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali leo Julai 15, 2024 uliofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi Rehema Madenge amesema ;-
“. Nitumie fursa hii kuipongeza Halmashauri hii ya Wilaya ya Namtumbo kwa Kupata Hati safi”.
Bi Rehema Madenge amewaelekeza Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji na Waheshimiwa madiwani kuendelea kusimamia na kuhakikisha hakuzalishwi hoja wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG Mwaka 2024/2025.
“Nataka wakuu wa idara wote washiriki kikamilifu katika suala zima la kuzuia uwepo wa hoja na kuzijibu hoja za ukaguzi, Endeleeni kusimamia vyema ili Hoja hizo kujirudia" :- Rehema Madenge,
Kikao hicho cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG kimefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Comments