MZEE WA MIAKA 63 AUWAWA MBOZI NA KUNYOFOLEWA VIUNGO VYAKE



Watu wasiojulikana wamemuuwa Mzee Kuminya Sambo (63) mkazi wa kijiji cha Nambizo wilayani Mbozi Mkoani Songwe huku viuongo vya mwili wake ikiwepo mguu na mkono vikiwa vimenyofolewa kandokando ya barabara.


Baadhi ya ndugu wa marehemu pamoja na majirani wamesema mauaji ya Mzee Sambo ambaye alikuwa akiishi bila mke  yamewashitua huku wakiomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kujuwa chanzo cha mauaji hayo.


Mwananchi imefika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na mtoto wa marehemu Jose Kuminya Sambo ambaye amesema baba yake alikutwa ameuwawa kandokando ya barabara baada ya kupotea nyumbani kwa takribani siki 3 na wananchi kumtafuta bila mafanikio.

Amesema Mzee Sambo alipotea nyumbani nyakati za usiku Julai 9, 2024 hali iliyopelekea wananchi kuungana kumtafuta kwa siku 3 bila mafanikio ambapo Julai 11,2024 walimkuta akiwa ameuwawa kandokando ya barabara huku mguu moj na mkono vikiwa vimenyofolewa.


Grace Sambo mtoto wa marehemu amesema baada ya baba yao kupotea walifika nyumbani kwao na kukuta hakuna dalili zilizoonyesha kama nyumba imevunjwa waliona kama kawaida au baba yao amesafiri lakini walishangaa amekuywa amefariki ,hivyo wanaliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Namanga kijijini hapo Jackson Ntembo baada ya kupewa taarifa za kupotea kwa Mzee Sambo tulianza kumtafuta na hatimaye kumkuta akiwa amefariki huku akiwa amekatwa mapanga kifuani,kichwani  kisha mguu mmoja na mkono vikiwa vimeondolewa.


"Daktari aliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na kukuta una majeraha manne ambayo yalisababishwa na kukatwa na kitu chenye nchakali, na Mimi kama kiongozi naliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo," amesema Ntembo. 


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Gallus Hyera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia wote waliohusika na mauaji hayo.

Hivi karibuni wilaya ya Mbozi imekumbwa na matukio ya mauaji licha ya kwamba baadhi ya wliohusika na baadhi ya mauaji wanashikiliwa na jeshi la polisi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE