NOEL MAGARI DALALI MWENYE NDOTO ZA KUWA BILIONEA MKOA SONGWE

 


Mkoa wa Songwe ni Mkoa kitinda mimba nchini Tanzania ambao uchumi wake umeonekana kukua kasi  na vijana wa mkoa wa Songwe wamekuwa ni Vijana wakuchakalika usiku na mchana ili kuweza kujikwamua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja.


Katika angaza angaza yetu tunakutana na kijana Noel Mzumbwe anaejulikana hivi sasa kama Noel Magari kutokana na kujikita katika biashara ya kuuza magari iliompa umaarufu mkoani Songwe na mikoa mbali mbali nchi Tanzania.


Ukishuka Mji mdogo wa Mlowo ulipo Wilayani Mbozi makao makuu ya mkoa wa Songwe bila shaka ukiuliza tu Noel magari lazima utaonyeshwa aidha ofisini kwake au kijiweni kakaa akiendeleza shughuli zake za udalali wa magari.


Akiongea na Mwandishi wetu magari kwanza ameishukuru serikali ya awamu sita chini yake na Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kuwajali Vijana na kuwapa mazingira rafiki ya kujitafutia ridhiki zao za halali ili mradi tu ulipe kodi ya serikali


"Ndugu mwandishi asingekuwa Samia sijui ningekuwa wapi maana Mazingira haya tulivu ya awamu hii ndio yamenifanya nami nionekane na kuaminiwa na watu kutokana na utulivu uliopo Tanzania nisipo mshukuru Samia sijui nimshukuru nani hapa Tanzania? Alihoji Magari


Aidha Magari amewasihi Vijana wa Mkoa wa Songwe kutumia fursa mbali mbali zilizopo mbele yao hususani Mkoa huu wa Songwe na kuwataka kuacha tamaa kwa kufanya mambo yasiofaa kwa Jamii na kwa Mungu pia.


Mwisho magari ameiomba serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo kuwapa vipaumbele vijana watafutaji Mkoa Songwe ili kuwasukuma mbele zaidi katika utafutaji wao.


Ili kuweza kujipatia gari lako au unauza gari lako wasiliana na Noel Magari

  +255 675 775 103

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE