POLISI WATAKIWA KUTUNZA AFYA YA AKILI
Naibu Balozi wa Ireland nchini MAGS GAYNOR amewataka askari Polisi kutunza afya ya akili jambo litakalowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Ameyasema hayo leo tarehe 19.07.2024 katika Shule ya Polisi Tanzania -Moshi wakati akifunga mafunzo ya siku tatu awamu ya pili ya kuwajengea uwezo watendaji wa madawati ya jinsia nchini wa namna ya kukabiliana na makosa ya unyanyasaji kingono hasa kwa watoto.
Aidha, Naibu Balozi huyo ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania lina jukumu la kuwalinda watoto na kwamba wako tayari kuendeleza ushirikiano baina ya Nchi ya Ireland na Tanzania katika kufanikisha hayo.
Naye, Kamishna wa Polisi jamii nchini, FAUSTINE SHILOGILE amewataka wahudhuriaji wa mafunzo hayo kuthamini kwa vitendo mchango wa muda na raslimali uliotolewa na wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka ubalozi wa Ireland kwa kwenda kuyafanyia kazi yote yaliyofundishwa.
Pia, amewataka kwenda kutoa elimu kwa watendaji wengine ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo ili kuwa na uelewa wa pamoja katika kushughulikia makosa ya namna hiyo
Comments