SAUTI YA SIMBA DAVID SILINDE KUANZA KUUNGURUMA JIMBONI TUNDUMA SIKU SABA KUANZIA LEO
Mbunge wa Jimbo Tunduma David Silinde ambae pia ni Naibu Waziri wa Kilimo anatarajia kuanza ziara ya siku saba za Jimbo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali jimboni mwake ikiwa sambamba na kufanya Mikutano ya hadhara lengo likiwa ni kuwaelezea Wanatunduma fedha za miradi mbalimbali walizopewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika Jimbo la Tunduma.
Katibu wa Jimbo wa Silinde Zamana Simkwai amesema leo Jumatano 10.07.2024 ndio Mbunge anaanza rasmi ziara yake na ataanzia kata ya majengo ambapo atafanya Mikutano miwili mmoja ikiwa Soko la kimataifa la mazao ambapo ataongea na wafanyabiashara wa mazao ili kuwasikiliza kero zao kisha jioni siku hiyo hiyo atakuwa soko la majengo pia kusikiliza kero na kuyaelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita.
Simkwai amewaomba Wananchi wa Jimbo la Tunduma kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya Mbunge na kuja na kero zao mbalimbali ili wazitatue kwa pamoja
"Mbunge wetu sauti ya Simba David Silinde amewataka Wananchi wa Jimbo la Tunduma wajitokeza kwa wingi kwani Wana jambo lao zito la siku saba Jimboni" amesema Katibu Simkwai.
Wakati huo Vijana wa Jimbo la Tunduma wamejipanga kumlaki sauti ya simba jimboni leo ambapo watampokelea ofisi za CCM Tunduma
Comments