WANACHAMA 80 WAIKACHA CHADEMA MOMBA
Wanachama zaidi ya themanini (80) wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Kamsamba Halmashauri ya Momba mkoani Songwe wamejiunga na CCM kwa madai kuwa wameridhishwa na utedaji kazi wa Serikali ya awamu sita inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakipokelewa mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Kamsamba na mbele ya Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe baadhi ya wanachama hao wamesema wameona hakuna haja ya kusalia Chadema, kwani CCM ya sasa chini ya viongozi wake wa Serikali wanafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Mmoja wa Wanachama hao ambao wamejiunga na CCM Joseph Simfukwe, ambaye pia amewahi kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Muungano kupitia tiketi ya CHADEMA, amesema kwa iyari ya moyo wake bila kushinikizwa na mtu yeyote ameona ni vema kurudi CCM ili kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita.
“Kwa kazi kubwa zinazofanywa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wetu Condester Sichalwe (Mundy) na diwani wetu Kyalambwene Kakwale, kwakweli tumekubali ya ishe ndiyo maana tumeamua sasa kurudi na kuungana na wenzetu kwenye utendaji kazi huu wa kuuwaletea maendeleo wananchi” Simfukwe.
Katibu wa CCM Kata ya Kamsamba Clemens Mapunda amesema mpaka kufikia leo amepokea majina zaidi ya 80 ya wanachama wa Chadema ambao wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM na kuna wanachama wengine wengi ambao wameonyesha nia ya kurudi CCM na siyo muda mrefu watapokelewa.
“Sisi kama CCM kata hii ya Kamsamba tumefarijika sana kuona wenzetu wa upande wa pili wamekubali mziki wetu na bili kusukumwa wameona wajiunge nasi, tumshukuru sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, wewe Mbunge Sichalwe na diwani wetu Kakwale, kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ambayo imeshawishi vyama vya upinzania kuanza kujiunga na chama chetu” Mapunda.
Kwa upande wao Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe na diwani wa kata ya Kamsamba Kyalambwene Kakwale, wamewakaribisha wanachama hao wapya, na kuwaomba waendelee kuwapa ushirikiano ili kutimiza ile adhima ya kuwapatia kuwatumikia wanananchi.
Comments