WATAALAMU KUTOKA ZHEJIANG NORMAL UNIVERSITY WAENDESHA MAFUNZO KWA WAKUFUNZI WA ADEM
Timu ya Wataalamu 11 ikujumuisha maprofesa na Madaktari kutoka Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University cha nchini China wamefika ADEM leo tarehe 9 Julai, 2024 kwa ajili ya ziara maalumu ikiwa ni hatua ya kuanza kwa utekelezaji wa mkataba wa ushirikiano ulioingiwa kati ya ADEM na chuo kikuu cha Zhejiang Normal University mnamo Mwezi Desemba, 2023 uliolenga kubadilishana utaalam, ufadhili wa masomo ya Muda Mfupi na Mrefu, kutembeleana ili kujifunza, kufanya tafiti nk.
Wataalamu hao wataendesha mafunzo ya siku tatu kwa Wakufunzi wa ADEM kuhusu Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu hasa eneo la Instructional Leadership na Uthibiti Ubora wa Elimu ili kuwajengea uwezo katika maeneo hayo.
Katika ufunguzi wa programu hiyo ya mafunzo, Dean college of Education ZJNU Prof. Huang Xiao ameshukuru Menejimenti ya ADEM kwa kukubali ushirikiano na Chuo Kikuu cha ZJNU ambao utaleta matokeo chanya kama pande zote mbili zilivyokubaliana namna ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitaaluma zitakazofanyika kupitia ushirikiano huo, hivyo amewataka wakufunzi wanaoshiriki mafunzo hayo kuyatumia kwa manufaa yao na elimu ya Tanzania kwa ujumla.
Aidha, Mtendaji Mkuu Dkt. Siston Masanja Mgullah akizungumza katika ufunguzi wa programu hiyo ya mafunzo amesema mafunzo hayo yatakayoendeshwa na wataalamu hao kutoka ZJNU ni utekelezaji wa mkataba wa ushirikiano ulioingiwa kati ya ADEM na chuo kikuu cha Zhejiang Normal University mnamo Mwezi Desemba, 2023 uliolenga kubadilishana utaalam, ufadhili wa masomo ya Muda Mfupi na Mrefu, kutembeleana ili kujifunza, kufanya tafiti nk.
Comments