WAZIRI JAFFO: TUTAHAKIKISHA TUNATATUA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA MIPAKANI

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema kuwa Wizara yake itahakikisha inatatua changamoto za kibiashara katika maeneo ya mipakani ili sekta ya viwanda na biashara iweze kukua 

Dkt. Jafo amesema hayo Julai 18, 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama kuwasalimia wananchi wa mji wa Tunduma Mkoani Songwe alipopita akitoka katika ziara yake Mkoa wa Rukwa


Amesema kuwa Wizara hiyo itahakikisha inatakeleza maagizo yaliyotolewa na utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema katika ziara ya Kitaifa nchini humo Oktoba 23 - 25, 2023 yanayohusu utatuzi wa changamoto za biashara katika mpaka wa Tunduma.


Aidha, Jafo amebainisha kuwa kati ya changamoto 15 zilizokuwepo katika mpaka huo, changamoto nne (4) tayari zimeshafanyiwa kazi huku akiahidi kuwa changamoto zingine zinaendelea kufanyiwa kazi.


Akifafanua zaidi, Dkt. Jafo amesema kuwa changamoto ya foleni ya malori iliyokuwa inasumbua katika mpaka wa Tunduma iliyotokana  na skana imetatuliwa baada ya Rais Samia kutoa skana moja kwa ajili ya upande wa Zambia.


Pia, Waziri Jafo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo kwa kutenga zaidi ya ekari 1,500 ambapo ekari 1000 ni kwa ajili ya bandari kavu na ekari 500 kwaajili ya ujenzi wa viwanda.


“Mkuu wa Mkoa (wa Songwe) nikuhakikishie tutafanya kila njia viwanda hivyo vitajengwa. Mheshimiwa Rais nikuhakikishie sisi Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na TRA pamoja na Forodha tutahakikisha vikwazo vyote visivyokuwa vya kikodi tuweze kuviondoa kwa lengo la kuhakikisha Tanzania hii inanufaika kwa suala la biashara” Amesema Dkt. Jafo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE