WIZARA YA AFYA YATOA TAMKO AGIZO LA RAIS TUNDUMA JUU YA MTOTO MLEMAVU
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema wao kama Wizara wamelipokea agizo la Rais Dkt Samia alilolitoa mapema leo asubuhi tarehe 18.07.2024 akiwa Mkoani Songwe katika Mji wa Tunduma kuhusu mtoto mwenye ulemavu wa miguu mmoja
"Tumepokea kwa ajili ya Utekelezaji mara moja Maelekezo ya Mhe Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu Mtoto Ebenezer Wile Mwaksyle (8) ambaye ni mlemavu kupatiwa huduma ya kutengenezewa Mguu Bandia, pamoja na huduma bora za afya.
Tunamshukuru Mhe Rais kwa upendo wake wa dhati na moyo wa huruma kwa wananchi wake" ameandika Waziri Ummy
Comments