CCM SONGWE YAWAONYA WABUNGE NA MADIWANI KUCHAFUANA MITANDAONI

 


Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe kimelaani vikali vitendo vya kuchafuana katika mitandao ya kijamii hususani mtandao wa Whatsapp kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na katibu  uenezi siasa na mafunzo Yusuph Ally imedai kuwepo kwa Viongozi,Madiwani,wabunge na wanachama wanatumia mitandao ya kijamii Mkoani Songwe kuchafuana kama taarifa inavyosomeka hii hapa.


 TAARIFA KWA UMMA


 HABARI ZENU WANACHAMA, MAKADA NA VIONGOZI WOTE WA CCM MKOA WA SONGWE!


Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe kinasikitishwa na kinalaani kampeni za kupakana matope baadhi ya waheshimiwa wabunge, madiwani na viongozi wa chama wa mkoa wetu wa Songwe zinazoendelea kwenye makundi songezi ya whatsap. *Jambo hili ni kosa la kukichafua na kukipaka matope chama kitu ambacho ni utovu wa nidhamu unaopelekea kwenye makosa ya maadili.* _Mijadala yote ya chama na hoja humalizwa kwenye vikao halali vya chama._ *Kwa muktadha huu, chama kinakemea na kupiga marufuku mijadala yote ya kupakana matope inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na kwa kweli chama hakitosita kumchukulia hatua za kinidhamu mwanachama na kiongozi yeyote wa CCM wa nafasi yoyote atakayeendeleza mijadala hii popote pale alipo.* Chama kiko makini na kinaendelea kulifuatilia kwa umakini na ukaribu jambo hili na kwa kweli (chama) hakitosita kuchukua hatua stahiki kwa kila anayehusika.

________________________

 Imetolewa na

Mwl. Yusuph Ally Rajab- Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM (M) Songwe.

Ijumaa ya tarehe 09/08/2024.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE