DC BUSEGA APIGWA MAWE


 Wakati baadhi ya Wananchi wakikiri kuwa kuna Watu kadhaa wanahofiwa kufariki kutokana na kupigwa risasi na Polisi wakijaribu kuwatawanya kwenye maandamano yaliyofanywa na Wananchi huko Busega Mkoani Simiyu leo, imethibitika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega Faiza Salim pamoja na Maofisa wengine wamejeruhiwa kwa mawe na Wananchi hao.


 imeelezwa kuwa Wananchi walimrushia Mkuu huyo wa Wilaya mawe wakati akiwasogelea kwa nia ya kuwasikiliza ambapo hawakutaka Kiongozi huyo kufanya chochote na kuanza kumrushia mawe yaliyopelekea kujeruhiwa kwenye ubavu na mgongoni huku Maofisa wengine aliokuwa ameambatana nao ambao ni Kamanda wa Zimamoto Simiyu na Kaimu Afisa wa TAKUKURU Simiyu wakijeruhiwa kichwani na kupelekea kushonwa nyuzi.


Kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata matibabu.


Wananchi wa Busega waliandamana leo hadi Kituo cha Polisi baada ya kuchoshwa na kushamiri kwa matukio ya Watoto wao kupotea katika eneo la Lamadi bila Polisi kuchukua hatua za kuridhisha kudhibiti matukio hayo

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE