DED MAGESA AUNDA TIMU NAMTUMBO YA KUFUATILIA NA KUTATHIMINI MIRADI KABLA YA MALIPO



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa ameunda kikosi kazi (Value for Money Audit Team) ambacho kimekuwa kikihusika na Ufuatiliaji na Kufanya Tathmini ya Miradi Mbalimbali kabla ya Kufanya Malipo.

"Uwepo wa kikosi kazi hiki cha Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi kabla ya Kufanya malipo (Value for Money Audit Team) inasaidia kufanya Malipo kwa Mkandarasi,Fundi au Mzabuni aliyekidhi Vigezo vya Mahitaji yetu na Si vinginevyo" - Amesema Magesa

Akizungumza Katika kikao kazi na Watendaji kata 21 za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Magesa amewataka watendaji kata Kuwa Makini na Miradi uku akizitaja Faida za kikosi kazi hicho cha Ufuatiliaji Miradi Kabla ya Malipo (Value for Money Audit Team) Ikiwa ni Kuhakikisha Mradi unatekelezwa kwa Viwango kama ilivyopangwa na Serikali.


pia kikosi kazi kitakuwa kinaangalia Vifaa na Mahitaji yanayo Nunuliwa kama yapo katika Mpango wa Mradi huo ili Mkandarasi,fundi au Mzabuni aweze kulipwa Stahiki kihalali.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE