DIWANI KYALAMWENE ATWAA UMAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA MOMBA


 Mhe. JOSHUA KYALAMBWENE MAKAMU MWENYEKITI MPYA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA.

Katika kikao cha Baraza Kuu la Madiwani la robo nne ya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wajumbe wa Baraza hilo walimchagua Mhe. Joshua kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri.


Katika uchaguzi huo Mhe. Joshua hakuwa na mgombea mwenza,amepigiwa kura zote za NDIYO sawa na asilimia 100 hivyo alitangazwa kuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.


Kikao hicho kilijumuisha wajumbe mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Mhe. Elias Mwandobo, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Fabian Manoza Said, Wakuu wa Tasisi mbalimbali, pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo.


Baada ya uchaguzi Mhe. Kyalambwene amewashukuru sana wajumbe waliomchawaliomchagua na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO