KASI YA WANAWAKE MAONYESHO YA NANE NANE MBEYA YAMVUTIA SENEDA


 Katibu tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda amekuwa ni mmoja kati ya Viongozi waliojitokeza katika maonyesho ya nane nane ya Kanda ya nyanda za juu kusini yanayoendelea Mkoani Mbeya leo tarehe 06/08/2024

Akiongea mara ya baada ya kutembelea mabanda ya wajasiliamali katika maonyesho  hayo amesema kuwa amevutiwa na kasi kubwa ya  Wanawake kujitokeza katika maonyesho na kutujenga nyesha ujasiliamali na kuitikia kwa nguvu tarajio la Rais Samia la kutaka wanawake kujitokeza katika fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi

"Nimeridhishwa sana na Wanawake kujitokeza katika maonyesho haya kuonyesha bidhaa mbalimbali za ujasiliamali hili ndio tarajio la Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hassani kuona Wanawake wanajikwamua kiuchumi" alisema Seneda


Maonyeshe ya nane Mkoani Mbeya yanatarajiwa kufungwa tarehe


08/08/2024


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE