MOLLEL ATAKA FEDHA ZA LISHE ZIWAFIKIE WALENGWA

 


Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesisitiza umuhimu wa kuzingatia lishe na matumizi sahihi ya fedha za lishe ikiwa ni kuwafikia walengwa husika wanaostahili kupata huduma hiyo


Dkt. Mollel ameyasema hayo Agosti 22, 2024, wakati wa Kikao kilichowakutanisha kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wadau wa lishe katika kuangali hali ya lishe katika mkoa wa Songwe ambapo hali ya lishe imekua nzuri tofauti na mwaka 2022/23 kwa kupanda hadi nafasi ya 7 kitaifa.


Aidha Dkt. Mollel amepongeza juhudi za mkoa wa Songwe katika kukabiliana na udumavu na kuzingatia lishe kwani lishe bora kwa watoto husaidia katika kukuza akili na hivyo kupelekea taifa lenye watu wenye weledi mzuri.


“Niwapongeze kwa juhudi hizi ambazo mmepitia, awali Songwe haikua vizuri kwenye lishe lakini kwa sasa mafanikio makubwa nimeyaona na hii itasaidia katika kukuza kizazi chenye akili kwani lishe husaidia katika ukuaji wa akili” Amesema Dkt. Mollel


Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amewataka wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi katika ngazi ya Wilaya kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa wanufaika ziende kwa wanufaika kama ambavyo imebainishwa asilimia 50 iliwafikia watoto chini ya Umri wa miaka 5


Mhe. Chongolo amesema kuwa mkoa wa Songwe umeingia katika mikoa yenye rekodi nzuri ya lishe hivyo kila mmoja awajibike katika kuhakikisha hali ya lishe inaendelea kuwa nzuri wakati wote kwa ajili ya kuwa na kizazi chenye makuzi mazuri na afya bora

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE