MTOTO MCHANGA AMEOKOTWA MTARONI TUNDUMA

Mtoto Mchanga anayekadiliwa kuzaliwa muda mfupi ameokotwa mtaroni katika mtaa wa Mpemba kata ya Mpemba Mjini Tunduma Mkoani Songwe akiwa ametelekezwa na mtu asiyefahamika baada ya kujifungua.

Wakizungumza  wananchi wa Shina 8 mtaa wa Mpemba Halmshauri ya mji Tunduma wamesikitishwa na kitendo cha Mtu asiyefahamika kutelekeza mtoto mtaroni baada ya kujifungua.REGINA KAMWELA mkazi wa Mpemba Tunduma,EUDIA KANDONGA mkazi wa Mpemba Tunduma na BENI SILINGWE Afisa usafirishaji Bodaboda


Amani Kandonga Balozi wa shina namba 8 Mtaa huo amethibitisha kuokotwa kwa mtoto huyo huku akilaani watu wanaofanya matukio ya kuzaa watoto na kutelekeza vichanga.


Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Halmshauri ya mji Tunduma Dkt Erasto Luvanda amekiri kupokea kichanga hicho kikiwa kimepigwa baridi kutokana na kukaa muda mrefu katika mtaro jambo lililopelekea kifo wakati kikipatiwa matibabu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

WAFANYABIASHARA SONGWE WALALAMIKA FOLENI YA KUSIMAMISHIA MAGARI SENJELE NA NANYALA WILAYANI MBOZI

CHONGOLO AWACHARUKIA RUWASA NA TANESCO KUTOSHIRIKI ZIARA YAKE