NAMTUMBO WATOA HUDUMA YA KUJIBU KERO ZA WANANCHI KUPITIA KURASA ZAO ZA MITANDAO
Halmashauri ya Namtumbo iliopo Mkoani Ruvuma imeazisha utaratibu wa kujibu maoni ya Wananchi wanayoyatoa kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa Halmashauri hiyo kitendo kinachonyesha ukomavu wa Viongozi wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Ngollo Malenya ambae ameoneka akiwajibu maoni yao kupitia ukurasa huo.
Philemon Magesa mkurugenzi wa halmashauri hiyo akiongea na mwandishi wetu amesema hao kama halmashauri kupitia mwongozo wa Sera ya matumizi bora, sahihi na salama ya mifumo na vifaa vya Tehama Serikalini ya mwaka 2014 ;
Sura ya 2 (1)(2) na (3) inayohusiana na kusimamia na kuendesha Tovuti ya Serikali na Mitandao ya Kijamii inasema: Kwa mujibu wa Mwongozo huu, Tovuti ni mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi na usambazaji wa habari, picha na nyaraka kwa njia ya mtandao. Mfumo huu pia unaweza kutumika kwa ajili ya kutoa mrejesho na huduma mbalimbali za Serikali. Mwongozo huu unahusu Tovuti, Tovuti kuu (portal), blogu na mitandao yote ya jamii. Wao wapo kutekeleza Sera na Mwongozo wa matumizi bora na sahihi mitandao.
"Sisi kama Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo tumeona Wananchi wetu walio wengi wanakuwa na Maswali, Hoja, Kero, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali. Kwa hiyo, Tumeamua kuandaa Jukwaa Maalum la Kukusanya, Kupokea na Kutoa Majibu kwa Wananchi wetu ili Kuwasaidia pia katika zoezi zima la kujua nini Serikali inafanya na nini pia Wananchi Wanaona katika nyanja zetu zote za Kiutawala"Amesema Magesa
Aidha amesema inawasaidia katika kurahisisha Mchakato wa usimamizi wa vipaumbele vya Halmashauri ambavyo ni Mapato, Miradi ya Maendeleo, na Utawala Bora. Halmashauri inafikisha taarifa na inapata mrejesho wa karibu kutoka kwa wananchi wao wanaowaongoza pia kuwa Karibu zaidi na Wananchina ikiwa ni pamoja na kuonesha Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wananchi katika Miradi mbalimbali tunayotekeleza na huduma tunazotoa kwa wananchi.
Magesa pia ametoa wito kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kutoa Ushirikiano katika Kutoa Taarifa lakini Kuuliza jambo lolote ambalo wao wanataka kulijua Kutoka Katika Halmashauri yao na sisi tutawapatia Ushirikiano wa kutosha katika Kuunga Mkono Jitihada za Rais wetu Mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo Katika Taifa letu la Tanzania.
Comments