RC MANYARA ATINGA NA KIVAZI CHA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDA

 


Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Agosti 14, 2024, ametembelea Shule ya mpya wasichana ya Manyara Girls na kuongea na wanafunzi pamoja na kuwakaribisha rasmi Mkoa wa Manyara wanafunzi 110 waliokwishawasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano (5) kwa mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB) shule hiyo iliyopo Kata ya Maiska Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara.


Mhe. Mkuu wa Mkoa, amewashukuru na kuwapongeza wazazi walioleta watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia watoto wao watapata Elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwepo shuleni hapo.


Sambaba na hilo RC Sendiga, ameagiza umaliziaji wa miundombinu yote ambayo bado haijakamilika ikamilike mapema ili wanafunzi waweze kupata huduma hizo hasa ya bwalo.

Comments

Popular posts from this blog

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14