WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SONGWE WASISITIZWA KURIPOTI HABARI ZINAZOELIMISHA JAMII MADHARA YA RUSHWA

 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewapa mafunzo  waandishi wa habari wa Mkoa wa Songwe ili kuwejengea uwezi wa namna ya kuepuka rushwa na kuelimisha jamii juu ya atheri za rushwa.


Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha uwezo wa waandishi katika kufichua na kuripoti rushwa katika sekta mbalimbali za umma na binafsi yametolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe, 

Frida Wikesi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.

      (Mwenyekiti wa krabu wa Waandishi wa habari Mkoani Songwe Stephan Simbeye akitoa neno)

Akitoa mafunzo hayo, Kamanda huyo amesema kuwa wanahabari ni kundi muhimu ambalo linaweza kusambaza elimu kwa jamii kwa haraka huku akiwasisitiza kuandika habari zinazoelimisha na kufichua vitendo vya rushwa.


"Tunaelekea kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, huku ndiko kunakolalamikiwa kuhusika na masuala ya rushwa nawaomba muandike habari za mapambano dhidi ya rushwa" amesema  Kamanda Wikesi na kuongeza;

    ( Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Takukuru Songwe)

"Rushwa ni dhambi. Tujitahidi kutumia kalqmu zetu kuelimisha jamii madhara ya rushwa. Kiongozi anapochaguliwa kwa kutoa rushwa hiyo ni kuwanyimq haki wananchi kwa miaka mitano na lazima atatanguliza mbele maslahi yake binafsi" amesisitiza Kamanda huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe

Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo waliiomba taasiai hiyo kuendelea kushirikiana nao ili kuboresha ufanisi katika kupiga vita dhidi ya rushwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE