ZEGE LAANZA KUMWANGWA ENEO LILILOKUWA MAARUFU KWA UPORAJI WAFANYABIASHARA BARABARA YA MLOWO-KAMSAMBA MKOANI SONGWW


Zoezi la kumwaga zege mlima wa Nyimbili maarufu kama Benki kuu barabara ya Mlowo Kamsamba limeanza kutekelezwa na Mkandarasi kupitia Wakala wa barabara Mkoa wa Songwe (Tanroads) ambapo sambamba na uwekaji wa zege hilo pia unaendana na upunguzaji wa ukali wa mwinuko katika mlima huo  maarufu kwa jina la benki kuu.


Eneo hilo ambalo lilijulikana zaidi miaka ya nyuma kama benki kuu kutokana na kuwa na Vitendo vya utekaji magari na uporaji  hali iliopelekea watu wengi kufanyiwa vitendo vya Ukatili na udhalilishaji ambapo Wadau wa njia hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwatengenezea zege hilo na kupunguza mlima.


"Kwa kweli tuna kila sababu ya kushukuru eneo hili kudhibitiwa kwani sisi madereva wa kamsamba eneo hili la benki kuu limekuwa eneo hatari kwa Usalama wa maisha yetu na abiria wetu tumetekwa sana na magari yetu tena mchana kweupe ndani ya msitu huu " amesema Emanuel Mwanga dereva wa fuso njia ya Kamsamba.


Baadhi ya wafanyabiashara wa Ng'ombe na Samaki nao wamepongeza uamuzi huo wa kumwagwa zege eneo hilo huku wakisema wao ndio walikuwa waathirika wakubwa wa kutekwa maeneo hayo na majambazi pindi Wanapogundua wametoka kwenye mauzo au kwenda kwenye manunuzi ya ng'ombe au samaki.


Meneja wa Tanroads Mkoa wa Songwe Injinia Suleiman Bishanga amesema wameamua kupunguza mlima Nyimbili maarufu kama benki kuu ili kupunguza ukali mlima huo na kuweka zege kutokana na magari kushindwa kupanda vizuri hivyo zege hilo litarahisisha na kupunguza tabu ya kuteleza pia zege hilo likekwenda sambamba na upanuzi wa barabara eneo hilo.


Aidha Meneja amesema barabara ya Mlowo Kamsamba ipo katika mchakato wa kuwekwa Lami na taratibu za mchakato huo zinaendelea kama kawaida.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE