CHONGOLO AWACHARUKIA RUWASA NA TANESCO KUTOSHIRIKI ZIARA YAKE
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo Amekasilishwa na kitendo cha Kutokuwepo katika ziara yake Tunduma kwa Wakuu wa Idara za RUWASA na TANESCO kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Katika ziara ya kikazi iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Tunduma, hali ya sintofahamu ilijitokeza baada ya wakuu wa idara muhimu za RUWASA na TANESCO kushindwa kufika ambapo Ambapo Chongolo alieleza kutoridhishwa kwake na kitendo cha viongozi hao kutohudhuria ziara hiyo na kumuagiza Katibu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda kuhakikisha Wakuu hao ziara zake wanakuwepo na kama hawawezi kusikiliza kero za Wananchi basi watafute Mkoa mwingine wa kufanya kazi.
Katika hotuba yake mbele ya maafisa na wananchi waliokuwepo, mkuu wa mkoa alisisitiza umuhimu wa viongozi wa taasisi za umma kuwajibika na kuheshimu ratiba za ziara za kikazi, hasa pale zinapohusisha masuala ya huduma za msingi kama maji na umeme, ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi. Alieleza kwamba kitendo cha kutokuwepo kwao kinaathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusababisha malalamiko kwa wananchi.
Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya jitihada za mkoa kuhakikisha huduma za maji safi na nishati ya umeme zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa viwango bora. Hata hivyo, kutokuwepo kwa wakuu wa idara hizo kulivuruga mipango ya ziara hiyo, na kuibua maswali juu ya uwajibikaji wa taasisi husika katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mkuu wa mkoa alionyesha nia ya kuchukua hatua stahiki kuhakikisha hali kama hiyo haijirudii na kutoa maagizo hayo kwa Katibu Tawala jambo hilo lisijirudie Ziara tena katika Ziara zake, na akawataka viongozi wa idara zote kuwa mfano wa uwajibikaji na ushirikiano katika kazi za maendeleo.
Kwa wananchi waliokuwepo, tukio hilo lilikuwa na umuhimu mkubwa kwani lilitoa ishara ya uwajibikaji wa uongozi wa juu na namna viongozi wanavyohusika moja kwa moja katika kufuatilia maendeleo na changamoto za kila siku zinazowakabili.
Comments