DED NAMTUMBO ATOA UFAFANUZI KUPUNGUA KWA IDADI YA VIJIJI TOKA 71 HADI 66

 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Namtumbo Philemon Magesa amesema kupungua kwa idadi ya Vijiji Wilaya ya Namtumbo inatokana na uwepo wa Miji Midogo ya Lusewa na Namtumbo hivyo kufanya idadi ya Vijiji Namtumbo kupungua


Akimjibu Mwananchi wa Namtumbo alieuliza swali kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Wilaya ya Namtumbo bwana Edson Ndunguru alitaka kujua kama idadi ya Vijiji 71 anavyovijua yeye vimepungua ama la? Ambapo Magesa ametoa ufafanuzi.


"Ni kweli kabisa kuna Vijiji  vimepungua kutokana na uwepo wa Miji Midogo ya Lusewa na Namtumbo kiutaratibu Kijiji au Kata inapopata hadhi ya kuwa Mji mdogo haiwezi kuwa na Kijiji hivyo Vijiji viwili  vilivyokuwa katika hizo Kata vilipunguzwa  Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imebakiwa na Vijiji 66 kutoka 71" amesema Magesa.


Mkurugenzi Magesa amewashukuru Wananchi wanaouliza maswali kupitia kurasa za Halmashauri ya Namtumbo na ameahidi kuendelea kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yatakayo ulizwa

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE