BARAZA LA MADIWANI MOMBA LATOA SHUKRANI KWA NAIBU WAZIRI SILINDE KWA KUSAIDIA MALIPO YA FEDHA KUTOKA NFRA


Baraza la Madiwani Momba Latoa Shukrani kwa Naibu Waziri Silinde kwa Kusaidia Malipo ya Fedha Kutoka NFRA


Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Momba limetoa shukrani za dhati kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa David Silinde, kwa jitihada zake zilizowezesha Halmashauri hiyo kulipwa fedha zao kutoka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).



Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Mathew Chikoti, Halmashauri ya Momba imelipwa jumla ya shilingi milioni 156.3 ikiwa ni ushuru wa mazao, pamoja na shilingi milioni 65.6 kama kodi ya pango kwa maghala matatu ya kuhifadhi nafaka kwa kipindi cha mwaka mmoja. Fedha hizi zilikuwa zikidaiwa kutoka NFRA na sasa malipo hayo yamekamilika kwa msaada wa jitihada za Naibu Waziri Silinde.


Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza hilo, Mwenyekiti Chikoti alieleza kuwa malipo hayo yameleta faraja kubwa kwa Halmashauri, na kuongeza kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha sekta ya kilimo na huduma za jamii katika Wilaya ya Momba.


“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, kwa kushughulikia madai yetu kwa NFRA. Kupatikana kwa fedha hizi ni hatua kubwa na muhimu katika kuchochea maendeleo ya kilimo na uchumi wa wilaya yetu," alisema Chikoti.


Baraza hilo pia lilitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi wa Serikali kuendelea kusaidia kutatua changamoto zinazokabili sekta ya kilimo, ili kuhakikisha wakulima wanafanya kazi katika mazingira bora na salama

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE