BIBI WA MIAKA 80 AONDOLEWA SHIDA YA UPUMUAJI NA MADAKTARI BINGWA WA SAMIA



Katika tukio la kusisimua, Bi. Maria Laureni (80), ameweza kuondokana na shida ya kupumua ambayo amekuwa akikabiliwa nayo kwa zaidi ya miezi nane baada ya kuhudumiwa na Madaktari Bingwa wa Samia walioko Mkoani Songwe.


Akiongelewa matibabu hayo, Daktari Bingwa kiongozi wa kambi Dkt. Manyasani Jisoli, amesema kwamba bibi huyo alikuwa katika hali ngumu kwa kipindi cha muda mrefu lakini kupitia huduma za kibingwa, wamemsaidia kuondokana na matatizo yake na hivi sasa anaweza kupumua kwa urahisi na kuendelea na shughuli zake za utafutaji.


Bi. Laureni alifika katika kambi hiyo akiwa na matatizo makubwa ya kupumua hasa nyakati za usiku akitaka kulala, hali ambayo imemfanya ashindwe kulala vizuri na kumfanya kutofanya vizuri katika shughuli zake za kujitafutia kipato.


Kupitia mpango wa Rais Samia wa kupeleka huduma za kibingwa na bingwa bobezi kwa jamii, madaktari bingwa na bobezi hao walifanikiwa kufanya uchunguzi na kupendekeza matibabu yaliyojumuisha mchakato wa kutoa maji yaliyokuwa yakikusanyika kwenye mapafu yake.


Kwa upande wake, Bi. Maria Laureni ameleza furaha yake kwa kusema amekuwa akipata shida kubwa ya kupumua zaidii ya miezi 8 lakini sasa anajihisi mpya.


“Naweza kurudi kwenye maisha yangu ya kila siku bila hofu, sisi kama Wakazi wa eneo hili tunampongeza RaiS Samia kwa juhudi zake za kutuletea madaktari bingwa na kutoa huduma za afya bora na za haraka katika maeneo yetu”. Amesema Bi. Laureni.


Kambi ya madaktari bingwa hii imekuwa na mafanikio makubwa, na inatarajiwa kufanyika kwa siku 7 katika maeneo mengine ya nchi ili kuweza kuwasaidia na kuokoa maisha ya watu wengi zaidi

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE