CHADEMA YASONONESHWA NA UANDIKISHWAJI TUNDUMA
WAKATI zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la mpiga kura kwa ajiri ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 likiendelea nchini kote, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Songwe kimelalamika kuchezewa rafu kwenye zoezi hilo katika jimbo la Tunduma.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo, ambaye ni msimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri hiyo, amekanusha malalamiko hayo na kusema yeye anasimamia sheria na kila chama kinatakiwa kufuata taratibu na shaeria zinazoongoza zoezi hilo litakaloambatana na uchaguzi wake hapo baadae.
Taarifa za Chadema kuchezewa rafu ziliibuliwa Oktoba14, 2024 na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Songwe, Isakwisa Lupembe, wakati akitoa taarifa za mwenendo wa zoezi hilo kwa waandishi wa habari.
Lupembe alitaja miongoni mwa mambo wanayolalamikia kwe ye zoezi hilo ni uandikishwaji kinyemela kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18, wakiwemo wanafunzi walio chini ya umri kutoka katika shule mbalimbali za sekondari katika Halmashauri na jimbo hilo.
"Tangu kuanza kwa zoezi hili, kumekuwa na matukio mbalimbali yanayoashiria ukiukwaji wa sheria, miongozo na taratibu, ikiwemo maofisa wa uandikishaji kuingiza kinyemela majina ya wananchi wasio na sifa ya kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi unaotarajia kufanyika hapo baadae na kila tunapojaribu kuwasilisha malalamiko yetu kwa Mkurugenzi (Chaurembo) amekuwa hataki kutusikiliza" alibainisha Lupembe.
"Baada ya ufuatiliaji tumebaini kuwa, mengi ya majina yanayochomekwa kwenye vituo mbambali vya uandikishaji ni majina ya wanafunzi na wengi wao wapo chini ya umri wa 18 ambao hawana sifa ya kuandikishwa na kushiriki kupiga kura" .
Alisema kuwa, majina hayo yamekuwa yakichukuliaa na kikundi maalumu alichodai ni makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao hutumia pikipiki kwenda mashuleni kukusanya majina hayo kisha huyapeleka kwa maofisa uandikishaji wa vituo na kuunganishwa kwenye orodha ya daftari la kituo .
Pia alitaja jambo lingine kuwa ni kuondolewa kwa mawakala wao katika vituo vitano vya kujiandikisha katika Halmashauri hiyo ya Tunduma licha ya kuwa na sifa.
Kutokana na malalamiko hayo, Lupembe amemtaka Waziri wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisem), Mohamed Mchengerwa kuingilia kati na kushughulikia malalamiko hao, ambayo wamedai yanaenda kinyume na kanuni na sheria ya zoezi zima la uandikishaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji Tunduma, Chaurembo akijibu malalamiko na tuhuma hizo, a
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo, ambaye ni msimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri hiyo, amesema malalamiko hayo si ya kweli na kwamba yeye anasimamia sheria na kila chama kinatakiwa kufuata taratibu na shaeria zinazoongoza zoezi hilo.
Kuhusu uandikishaji watu walio chini ya umri wa miaka 18, wakiwemo wanafunzi walio chini ya umri huo si za kweli na kwamba hata kama itatokea kuna mtu ameandikishwa akiwa chini ya umri huo bado vyama na wananchi wanafursa ya kuweka pingamizi mara baada ya zoezi hilo kukamilika na kutakuwa na siku mbili za kuweka mapingamizi baada ya orodha yote kubandikwa kituoni.
Akizungumzia kuhusu mawakala wa Chadema kuondolewa, Chaurembo alikiri kuonsolewa kwa mawakala watano wa chama hicho kwa kuwa hawakuwa na sifa, kwani kulitokea mbadilishano wa mawakala hao kinyume na taratibu.
"Mfano kuna kituo kimoja cha Katete kulijitokeza changamoto kwani wakala aliyefika siku ya kwanza ya uandikishajibsio yule aliyeapa, hivyo kwa mazingira hayo tuliwatoa hadi pale changamoto ilipopatia ufumbuzi" alifafanua Chaurembo.
Kutokana na hali hiyo, Chaurembo alitoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha kuwa vinafuata taratibu katika kipindi chote cha zoezi la uandikishaji, ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha.
Hata hivyo, Chaurembo alisema zoezi la uandikishaji kwenye Halmashauri hiyo linaendelea vizuri kwani hadi kufikia sasa jumla ya wananchi 39,361 tayari wamejiandikisha kutoka katika vituo vyote 196 vilivyopo katika Halmashauri hiyo.
Comments