DC MBOZI APANDA GUTA KUHAMASISHA WANAMBOZI KUJIANDIKISHSMA DAFTARI LA MPIGA KURA











Oktoba 2024 - Mlowo, Mbozi


Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Mahawe, ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Mbozi, hususani wakazi wa Mlowo, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.


Akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Mlowo, Mkuu wa Wilaya alisisitiza umuhimu wa kila raia aliye na sifa kuhakikisha amejiandikisha ili kupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi. Alieleza kuwa ushiriki wa wananchi ni msingi muhimu wa maendeleo na demokrasia, huku akiwakumbusha kuwa uamuzi wa viongozi wa mitaa unategemea kura zao.


"Nawaomba mujitokeze kwa wingi katika zoezi hili la kujiandikisha, kwani ni haki na wajibu wetu kama wananchi. Kupiga kura ni moja ya njia kuu ya kushiriki katika maendeleo ya wilaya yetu," alisema Bi. Mahawe wakati wa kampeni hiyo ya hamasa.



Aidha, Mkuu wa Wilaya alisisitiza kuwa Serikali ya Wilaya imejipanga kikamilifu kuhakikisha zoezi la kujiandikisha linafanyika kwa ufanisi, huku ikitoa wito kwa wananchi kufuata maelekezo ya viongozi na watendaji katika maeneo yao. Pia, aliwahakikishia kuwa Serikali itaweka mazingira salama na rafiki kwa wote watakaoshiriki zoezi hilo.






Wananchi waliohudhuria mkutano huo walionyesha hamasa kubwa, wakiahidi kushiriki kwa wingi katika mchakato huo wa kujiandikisha, huku wakiahidi kuhamasishana kwa wenzao ili kuongeza idadi ya wapiga kura.


#MboziInajitokeza #Uchaguzi2024 #KujiandikishaKwapigaKura

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE