IRAN YAISHAMBULIA ISRAEL USIKU ZAIDI YA MAKOMBORA 400


Jeshi la Iran limefyatua makombora zaidi ya 400 usiku huu kuilenga Israel na kusema imefanya hivyo ili kulipa kisasi kufuatia Israel kumuua Kiongozi wa Hamas na Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah Septemba 28 2024 ambaye alikuwa Mshirika wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Al Khamenei.


Rais wa Marekani Joe Biden ameingilia kati na kuliagiza Jeshi la Marekani kuisaidia Israel kuyadungua makombora hayo ambapo hadi sasa Israel imesema tayari baadhi ya makombora yamedunguliwa.


Nasrallah ameongoza kundi la Hezbollah tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 na alilibadilisha kundi hilo kuwa Jeshi ubwa la Kisiasa na Kijeshi, alikuwa Mshirika wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na adui mkubwa wa Taifa la Israel kabla ya kuuawa katika shambulio la anga la Israel ambapo baada ya kifo chake Israel ilisema Nasrallah alikuwa mmoja wa Maadui wakubwa wa Taifa la Israel wa wakati wote na kuondolewa kwake kunaifanya Dunia kuwa mahali salama, mauaji na kauli hiyo vimeikasirisha Iran na kuapa kulipiza kisasi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE