ISRAEL YASEMA IRAN ITAJUTIA KUWASHAMBULIA


Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Iran itateseka kwa shambulio lake usiku wa kuamkia leo ambapo Takriban makombora 200 yamerushwa hadi Israel kutoka Iran, kwa mujibu wa jeshi la Israel

 

Vikosi vya kijeshi vya Iran vimejibu vitisho hivi kutoka kwa maafisa wa Israel na vimesema Israel itapata "uharibifu mkubwa" wa miundombinu yake ikiwa itashambulia.


"IIran ilifanya kosa kubwa usiku wa leo, na italipia" - amesema Netanyahu, Washirika wa Israel wamelaani shambulio hilo, huku Eais wa Marekani Joe Biden akisema anaiunga mkono kikamilifu Israel


Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya wamerejelea wito wa kusitisha mapigano, huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kukutana Jumatano wiki hii.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE