RC CHONGOLO NA TRA WAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA UCHUMI NA KUDHIBITI MAGENDO SONGWE



Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo. Katika ziara hiyo, Mwenda alieleza malengo yake ikiwa ni pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo na kushirikiana kwa karibu katika ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa bidhaa za magendo mipakani.

Kwa upande wake, Mhe. Chongolo ameahidi ushirikiano na TRA, huku akieleza mikakati ya mkoa katika kukuza uchumi na kuvutia uwekezaji katika sekta za biashara, madini, na uchukuzi.


 Aidha, amepongeza mameneja wa TRA wa Mkoa wa Songwe kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafanyika kwa ufanisi.









Comments

Popular posts from this blog

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14