MADIWANI WAPITISHA AZIMIO KUZIITA SHULE MAJINA YA DC NA DED WA SONGWE KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUIMARISHA MAHUSIANO NA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Songwe limepitisha azimio la kuzipa majina ya Solomon Itunda (Mkuu wa Wilaya ya Songwe) na CPA. Cecilia Kavishe (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe) shule mbili mpya ambazo ujenzi wake umeanza, ikiwa ni kutambua mchango wa viongozi hao wa kuimarisha mahusiano katika wilaya hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.


Azimio hilo limepitishwa leo Jumanne Oktoba 22, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Sambila uliopo katika ofisi za Halmashauri.

Azimio hilo limepitishwa baada ya madiwani kupata nafasi kila mmoja kujadili sababu za kuzipa shule hizo majina ya viongozi hao, wakieleza kuwa wamekuwa wakiimarisha mahusiano na kusababisha Wilaya kuwa na utulivu pamoja na usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Katika azimio hilo, Shule ya Amali inayojengwa katika kijiji cha Iseche Kata ya Mwambani ambayo inaghjarimu Sh1.6 bilioni itaitwa Itunda (Solomon Itunda) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe huku Shule ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Kimborokoto Kata ya Mkwajuni itakayogharimu Sh583 milioni ikipendekezwa kuitwa Cecilia Kavishe ambalo ndilo jina la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE