MKULIMA AWAUA WANAWAKE WAWILI KISHA MIILI YAO AWAPATIA NGURUWE



Kisa cha wanawake wawili weusi wanaodaiwa kupigwa risasi na miili yao kupewa nguruwe wale na mfugaji mzungu na wafanyakazi wake wawili kimezua taharuki nchini Afrika Kusini.

Maria Makgato, 45, na Lucia Ndlovu, 34, inaelezwa walikuwa wakitafuta chakula katika shamba hilo karibu na Polokwane katika jimbo la kaskazini mwa Afrika Kusini la Limpopo mwezi Agosti walipopigwa risasi.

Miili yao ilipewa nguruwe ili kuila katika jaribio la kuondoa ushahidi.

Mahakama sasa itaamua kama itatoa dhamana kwa mmiliki wa shamba hilo Zachariah Johannes Olivier, 60, na wafanyakazi wake Adrian de Wet, 19, na William Musora, 50, kabla ya kesi yao ya mauaji.

Wanaume hao watatu bado hawajaombwa kuwasilisha ombi la dhamana, jambo ambalo litafanyika kesi itakapoanza baadaye.

Katika vikao vya awali vya kesi hiyo, waandamanaji wameandamana nje ya mahakama wakitaka washukiwa wanyimwe dhamana.

Nduguye Bi Makgato, Walter Mathole ameambia BBC tukio hilo limezidisha mvutano wa kikabila kati ya watu weusi na weupe nchini Afrika Kusini.

Mivutano ya wazungu na watu weusi imeenea sana katika maeneo ya vijijini, licha ya kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi miaka 30 iliyopita.

Katika mahakama ya Polokwane, wanaume hao watatu katika pia wanakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumuua kwa kumpiga risasi mume wa Bi Ndlovu, ambaye alikuwa pamoja na wanawake hao shambani – na kesi ya kumiliki bunduki isiyo na kibali.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE