SERIKALI KUANZA UJENZI WA BARABARA YA NJIA SITA DODOMA
Serikali inatarajia kuanza Ujenzi wa barabara ya njia 6 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma itakayounganisha Jiji hili na miundombinu mingine ya usafirishaji ikiwemo uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato, Reli ya SGR na barabara ya Mzunguko( Ring road) ili kupunguza msongamano katikati ya Jiji.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 02,2024 na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ameeleza juu ya mpango huo Jijini Dodoma, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje yenye Urefu wa Kilomita zaidi ya 112 ambapo amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na Mazungumzo na Benki ya Dunia ili kuwezesha Utekelezaji wake.
Barabara hizo zitajengwa kwa mwelekeo wa mikoa yote minne inayopakana na Dodoma ambayo ni Morogoro,Dar es salaama, Manyara, Arusha, Singida,Mwanza na Iringa na Mbeya.
Kuhusu Mradi huo wa barabara ya Mzunguko “Outer Ring-Road “ Waziri Bashungwa amesisitiza wakandarasi kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ya Mkataba na kwamba Serikali haitoongeza muda wa ukamilishaji wake.
Mradi wa Barabara ya Mzunguko unatekelezwa kwa vipande viwili ambapo Msimamizi kutoka wakala ya Barabara Tanzania TANROADS Mhandisi Herman Laswai na Mshauri Elekezi katika mradi wa kipande cha kwanza wameeleza kusimamia mradi kwa karibu ili uweze kukamilika kwa wakati.
Katika ziara hiyo Mhe. Bashungwa aliambata na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule pamoja viongozi wengine ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Dodoma jiji .
Comments