UHABA WA KONDOMU WILAYANI MOMBA WAZUA WASIWASI WA MAAMBUKIZI YA VVU

 

Diwani wa Kata ya Mpapa, wilayani Momba, George Kansonso, amelalamikia uhaba wa kondomu katika kata yake, akisema kuwa hali hiyo inaongeza hatari ya maambukizi mapya ya VVU na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kansonso alieleza wasiwasi huo mbele ya Baraza la Madiwani na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha upatikanaji wa kinga hizo.

Akijibu malalamiko hayo, Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Momba, Haroub Almas, alisema kuwa wilaya hiyo inatarajia kupokea kondomu 54,000 kama hatua ya awali, na idadi hiyo itaongezwa pindi zitakapopatikana zaidi. Almas aliongeza kuwa kondomu hizo zitasambazwa katika maeneo yote muhimu, lengo likiwa ni kuwafikishia wananchi kwa urahisi.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Mathew Chikoti, aliunga mkono juhudi hizo lakini akashauri kuwa usambazaji wa kondomu ufanyike kwa umakini. Alisisitiza kuwa kondomu hazipaswi kuachwa kwenye maeneo ya hospitali pekee, kwani hospitali ni mahali pa kutibiwa na si kwa ajili ya kuchukua kinga. Badala yake, alishauri kondomu ziwekwe katika sehemu za starehe na maeneo yanayofikika kwa urahisi ili kuweza kuwahudumia wananchi ipasavyo.



Wilaya ya Momba inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto za maambukizi mapya ya VVU kwa kuhakikisha upatikanaji wa kondomu, hasa katika maeneo yenye mahitaji makubwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE