WABUNGE WAUNGA MKONO MAKAMU WA RAIS KUTIMULIWA

 


Wabunge nchini Kenya jioni hii wameanza mchakato wa kumwondoa madarakani Makamu wa Rais wa nchi hiyo ofisini.


Wanamshutumu Rigathi Gachagua kwa madai kwamba alihusika na maandamano ya vurugu yaliyotokea nchini Kenya miezi mitatu iliyopita.


Pia wanadai kwamba Gachagua anahusishwa na ufisadi, kudhoofisha serikali na kukuza siasa za mgawanyiko wa kikabila.


Ruto alimteua Gachagua kama mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa mwaka 2022, ambapo alimshinda Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.


Gachagua anatoka katika eneo la Mlima Kenya ambako kura ni nyingi zilitoka, na alisaidia kwa kiwango kikubwa kumfanya Ruto kupata uungwaji mkono huko.


Lakini baada ya wanachama wa chama cha Odinga kujiunga na serikali kufuatia maandamano yaliyoandaliwa na vijana (Gen Z), ambayo yalimlazimisha Ruto kusitisha ongezeko la kodi, hali ya kisiasa nchini imebadilika. Makamu hiyo wa Rais ameonekana kujitenga zaidi huku yeye akidai anatengwa na watu wa Ruto.


Mbunge wa Kibwezi Mashariki, Mwengi Mutuse ndiye amewasilisha hoja ya kumwondoa ofisini Gachagua jioni hii.


Kwa mujibu wa kifungu cha 150 cha Katiba, hoja ya kumwondoa Makamu wa Rais inapasa kuungwa mkono na angalau thuluthi moja ya wabunge wote, kabla ya Spika wa Bunge la Kitaifa kuruhusu ijadiliwe. Hiyo ni sawa na wabunge 117 kati ya 349.


Gachagua amekuwa akisema si rahisi kumwondoa madarakani kutokana na kuchaguliwa na Wakenya wengi sambamba na Rais Ruto.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE