BARAZA LA MADIWANI LAWAPONGEZA WALIMU UFAULU WA DARASA LA SABA



Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi limewapongeza wanafunzi wa darasa la saba kwa kufanya vizuri na kuazimia kianzisha programu za mitihani ya wiki ikiwa ni mkakati wa kupandisha kupandisha ufaulu.

Akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la kupokea taarifa za Kata Mwanyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mhe. George Musyani amesema kuwa jitihada zilizofanywa na wataalamu kupandisha ufaulu zinatakiwa kutiliwa mkazo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.  

"Tutengeneze mkakati ambao tutakwenda nao mpaka mwakani ili watoto wetu wafaulu zaidi. Nawashukuru walimu kwa jitihada zao zilizowafanya wanafunzi hao kuongeza ufaulu kutoka asilimia 74 mpaka asilimia 81" amesema na kuongeza;


"Twendeni kianzisha programu za mitihani ya kila mwisho wa wiki ambayo inaweza kufanyika kwa kushindanisha shule kwa shule ambayo itawafanya wasome kwa bidii. Tujitahidi kwenda kutoa elimu kwa wananchi wetu kuhusiana na suala hili ili wote tuwe na uelewa wa pamoja ili kusitokee manunguniko ndani ya jamii" amesisitiza.


Mhe. Musyani amewataka madiwani hao kwa kushirikiana na watendaji, waratibu elimu kata pamoja na polisi kata kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari wanajiunga wote.

Akichangia katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Bara Mhe. Mndalavuama ameshauri kuwa  Halmashauri hiyo ianze mpango wa ujenzi wa mabweni  ili kudhibiti utoro wa wanafunzi.





Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE