MKURUGENZI DAR 24 MEDIA AKANA KUTEKWA ADAI NI WEZI WALITAKA KUMUIBIA FEDHA NA WALIMLEVYA
Mkurugenzi Mtendaji wa Television inayotoa habari mitandaoni ya Dar 24 Media ambaye pia ni Mtendaji wa Data Vision aitwaye MacLean Godfrey Mwaijonga ambaye alipotea tangu October 31,2024 alipotoka ofisini saa 11 jioni, amepatikana jioni ya leo November 02,2024 eneo la Buyuni Wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam ambapo amesema hakutekwa bali Wafanyabiashara wenzake walimlevya na wakapanga kuiba pesa zake na vitu vingine.
Akiongea na Ayo TV usiku huu mbele ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Jumanne Muliro na Familia yake Central Police Dar es salaam, MacLean amesema hakutekwa maeneo ya ofisini kwake bali alienda mwenyewe Kigamboni kukutana na Wafanyabiashara wenzake anaowafahamu ili wafanye maongezi ya kibiashara lakini wakamuwekea dawa za kulevya kwenye juisi na akapoteza fahamu na alipozinduka wakaanza kumshinikiza awape password za benki na za mitandao ya kampuni anazozisimamia “Walinitoa pale nilipokuwa ambap sipafahamu na wakaniweka kwenye gari na kuanza kunizungusha wakidai walichotaka niwape walipoona hawapatii wakaniacha Buyuni”
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa taarifa za kupatikana kwa MacLean alizipata kutoka kwa Baba Mzazi wa Kijana huyo ambaye alipigiwa simu na Msamaria mwema kuwa wamemkuta MacLean Buyuni ambapo alitelekezwa na wenzake na wakiwa na Polisi wakiwa na Ndugu zake walienda mpaka maeneo ya Kigamboni, Buyuni na kumkuta akiwa barabarani anapepesuka kisha walimpeleka Hospitali na baada ya vipimo ilionekana ana afya njema.
Comments