MWILI WA BINTI ALIEBAKWA Rucu WAZIKWA KWAO ILEJE


 Mwili wa Rachael Mkumbwa wazikwa Ileje


Baba mzazi wa marehemu aliangukia jeshi la polisi


Denis Sinkonde.,Mwananchi

Denissinkonde@mwananchi.co.tz


Ileje. Wakati mwili wa Rachael Mkumbwa ukizikwa leo katika kjiji cha

Isongole kata ya Isongole wilayani Ileje Mkoani Songwe baba mzazi wa binti huyo Dickinson Mkumbwa ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwakamata waliohusika kuhusika na mauaji hayo.


Dickinson Mkubwa amesema licha ya mwanangu kuzikwa Leo naiomba serikali kupitia jeshi la polisi lifanye uchunguzi kuwabaini na kuwakamata wahusika wote ili Sheria ifuate mkondo wake na kukomesha vitendo vya ubakaji.


Amesema unyama aliofanyiwa mwanae ni kitendo ambacho hakivumiliki kwani mwanae alikuwa akiishi kwa kumtumikia Mungu lakini amefariki katika mazingira ambayo hayastahikili mioyo yetu.


Mkumbwa amesema kama familia wanategemea jeshi la polisi na serikali katika upelelezi ambao utasaidia kuwakamata waliohusika kutenda unyama huo kwani familia ya Racho imeumizwa na taarifa za kifo cha mtoto wao.


Mkumbwa amesema ninajuwa kifo kipo lakini si kwa stahili ya kifo cha mwanangu, tunaaamini vyombo vya usalama vitafanya kazi yake ,kwani kwa kipindi hiki tunashindwa kuzu gumza mengi zaidi kwani shetani mlaniwa amefanya kitendo ambacho hakivumiliki


"Nilisafiri kutoka Ileje mpaka Iringa baada ya taarifa ya kifo cha mtoto wangu kwa kweli inaumiza ndoto ya mwanangu imeishia hapa siwezi kuzungumza chochote naishia hapa mwandishi tumwachie mungu," amesema baba mzazi wa Marehemu Mkumbwa.


Kwa upande wake moja wa mwanafamilia Hamisi Mkumbwa amesema kifo cha mdogo wao Rachel Mkumbwa kiliwashitua sana kwani walikuwa wanasikia mbali aina ya mauaji hayo hivyo tuombe uchunguzi wa jeshi la polisi ufanyike Kwa kina kuwakamata wahusika wote.


Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa Desemba 13 na kamanda wake SACP, Allan Bukumbi imeeleza kuwa marehebu alibakwa kisha watuhumiwa kuchukua simu yake ya mkononi.


“Tukio hili lilitokea Desemba 12 saa 5 usiku, ambapo upelelezi umebaini watuhumiwa waliingia cha jirani ambaye naye ni mwanafunzi na kuchukua simu mbili na laptop,”


Wasifu wa marehemu

Marehemu Rachel Mkumbwa alizaliwa February 17,2005 katika Kijiji Cha Malangali wilayani Ileje, alisoma shyle ya msingi Ilulu kuanzia mwaka 2010 mpaka 2016, shule ya sekondari Consolata kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020 na elimu ya kidato Cha Tano na sita katika shule ya sekondari Ileje kuanzia mwaka 2021_2023


Mpaka umauti unamkuta marehemu  Desemba 12,2024 alikuwa akisona katika chuo Cha RUCU Kituvo cha Teknolojia ya habari na mawasiliano akichukua shahada ya sayansi  ya elimu katika masomo ya    IT na Hesabu0


Rachel alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu, RUCU mkoani Iringa, alikutwa amefariki dunia nyumbani kwake Desemba 12 kwa madai ya kubakwa hadi kuuawa.


Comments

Popular posts from this blog

ASKARI WATATU KITUO CHA TUNDUMA MAHAKAMANI KWA KWA RUSHWA

MFANYAKAZI NMB AFARIKI KWA KUJINYONGA