KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

Tarehe ya Kuzaliwa: 05 Novemba, 1973 Mahali: Kijiji cha Isale, Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara ELIMU Mh. Ester Alexander Mahawe alianza safari yake ya elimu katika Shule ya Msingi Upper Kitete, Wilaya ya Karatu mnamo 1982-1983 na baadaye kuhamia Shule ya Msingi Isale, ambako alihitimu mwaka 1988. Alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Imboru, Wilaya ya Mbulu kati ya mwaka 1989-1992. Mnamo 1994-1996, alihitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kutoka Chuo cha Ualimu Monduli, Mkoa wa Arusha. Mwaka 2012-2013, alihitimu stashahada ya Uongozi na Utawala kutoka Chuo cha ESAMI, Mkoa wa Arusha. NDOA NA FAMILIA Mnamo tarehe 17 Septemba 2005, Ester Alexander Mahawe alifunga ndoa na Alexander Samson. Ndoa yao ilijaliwa watoto watatu wa kuwazaa: wavulana wawili na msichana mmoja. Aidha, aliwalea watoto wengine sita na hivyo kuacha jumla ya watoto tisa pamoja na wajukuu tisa. KAZI NA UZOEFU Huduma ya Ualimu: 1996-1997: Mh. Ester alikuwa mwalimu katika St. Constantine International Sch...