Machapisho

KAMANDA WA POLISI AJIUZULU

Picha
  MKUU wa Polisi wa kitaifa wa Japan, Itaru Nakamura amewasilisha ombi la kujiuzulu baada ya kukiri kushindwa kumlinda Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe ambaye aliuawa hivi karibuni wakati wa kampeni ya uchaguzi.   Nakamura ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa wameamua kupanga upya timu yao na kuanza misheni za usalama. Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe Shinzo Abe alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi Julai 8, 2022 wakati wa kampeni ya uchaguzi katika eneo la Nara lililopo Magharibi mwa Japani.   Mtu anayeshukiwa na mauaji hayo, Tetsuya Yamagami alikamatwa katika eneo la tukio na kwa sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiakili hadi mwisho wa mwezi Novemba mwaka huu.   Yamagami aliwaambia polisi kwamba alifanya tukio hilo baada ya mama yake kuchangia pesa nyingi kwake na kumsababishia umasikini.   Siku moja baada ya kuuawa kwa Shinzo Abe, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Nara, Tomoaki Onizuka aliki...

MABILIONI YAPELEKWA JESHI LA POLISI KUNUNUA MAGARI YA MAKAMANDA

Picha
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amesema, Serikali imetoa Sh15 bilioni kwa ajili ya kununua magari yatakayopelekwa kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa (Ma-RPC). Aidha, magari hayo yatakwenda kwa makanda wa polisi wa wilaya (Ma-OCD) na fedha ya mafuta itakayokwenda moja kwa moja wilayani ili kurahisisha utendaji kazi za Polisi. Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Agosti 25, 2022 na Waziri Masauni wakati anafunga mafunzo awali ya polisi kozi namba moja ya 2021/2022 katika Shule ya Polisi Tanzania, Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Waziri huyo amewataka askari wahitimu kuwaheshimu Watanzania ikiwa ni pamoja na kutenda haki sambamba na kuyashughulikia matukio ya uhalifu kwa wakati na kwa haraka. Kwa upande wake, Mkuu  wa Shule ya Polisi Tanzania, Ramadhani Mungi amesema shule ilipokea zaidi ya wanafunzi 4,310 na waliohitimu mafunzo hayo ni 4,122 huku wengine 186 wakiachishwa  mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu. Aidha, wahitimu hao wamejifunza...

UTEUZI:KAMISHINA MAGEREZA

Picha
 

SOMA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO

Picha
 

AZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KULEWA KUPINDUKIA AZINDUKA NA KUJIKUTA KABURINI

Picha
  MWANAUME mmoja anayefahamika kwa jina la Victor Hugo Mica Alvarez (30), mkazi wa Amerika Kusini ya Bolivia, amejitokeza na kueleza jinsi alivyoishia kuzikwa akiwa hai ndani ya jeneza baada ya kulewa kupita kiasi.   Mwanaume huyo alishtuka na kujikuta yuko ndani ya jeneza katika shimo lenye urefu wa futi sita chini ya ardhi baada ya kuzimia katika jiji la El Alto nchini Bolivia.   Inadaiwa, Alvarez alikunywa pombe nyingi usiku uliopita katika ufunguzi wa tamasha la Pachamama (tamasha la Mama Duniani), ambapo watu hutoa shukrani kwa miungu.   Alvarez anaamini kwamba wafuasi waliokuwa katika tamasha hilo, walimzika akiwa hai kama sadaka yao kwa mungu wa kike ambapo huamini kwamba, mungu wa kike hufungua kinywa chake kwa ajili ya kupokea matoleo yao kila ifikapo Agosti. Kaburi la Victor Hugo Mica Alvarez (30) “Jana usiku ilikuwa ni kipindi cha kabla ya tamasha, tulikwenda kucheza na baadaye, sikumbuki. Kitu pekee ninachokumbuka ni kwamba nilifikiri nilikuwa kitandani k...

MTOTO WA MBUNGE AFARIKI KWENYE SWIMMING POOL AKIOGELEA

Picha
  CELLIE Mwambe (14), ambaye ni mtoto wa Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe, amefariki dunia jana Agosti 23, 2022, baada ya kujirusha kwenye swimming pool ya nyumbani kwao maeneo ya Ada Estate Kinondoni Dar es Salaam, wakati akicheza na wenzake na kujigonga chini.   Akizungumza hii leo Agosti 24, 2022, kuhusu tukio hilo, mbunge huyo amesema kwamba, mtoto wake huyo baada ya kujirusha alienda upande wenye kina kidogo na kujigonga chini na kwamba alichelewa kutolewa majini ili kupelekwa hospitali.   “Hakukuwa na watu wazima karibu hivyo akanywa maji mpaka walipokuja kumuokoa ikawa ‘late’. Walivyomfikisha hospitalini ikashindikana kumuokoa, alifia hospitali baada ya kuwa amekunywa maji mengi nadhani hata pale alipojigonga alipata jeraha kubwa,” amesema Mbunge Mwambe.   Mwili wa marehemu Cellie unatarajiwa kuzikwa keshokutwa, Ijumaa, Agosti 26, 2022, jimboni Ndanda mkoani Mtwara

SOMA VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO

Picha
 

KARANI WA SENSA AJIFUNGUA KABLA YA KUANZA KAZI

Picha
  Karani wa Sensa ya Watu na Makazi wilayani Bunda mkoa wa Mara amejifungua muda mfupi kabla ya kuanza kazi hiyo, hivyo kulazimika kuondolewa kwenye orodha ya makarani katika wilaya hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari amesema kuwa karani huyo amejifungua usiku wa kuamkia Agosti 23, 2022 ingawa hakuweza kumtaja jina. "Tangu tumeanza tumepata changamoto ambayo pia ni baraka kuna karani wetu amejifungua usiku na bahati nzuri alijifungua kabla ya saa sita kwahiyo yeye na mtoto wake pia wamehesabiwa na baada ya hali hiyo kujitokeza tayari karani wa akiba ameshachukua nafasi na kazi inaendelea," amesema Nassari. Amefafanua kuwa wilaya ya Bunda inao makarani zaidi ya 1,000 na kwamba shughuli ya kuhesabu watu na makazi inaendelea na huku akiamini kuwa kazi hiyo itakamilika kwa ufanisi. Amewataka wakazi wa Bunda kutoa ushirikiano kwa makarani na kutoa taarifa sahihi zitakazowiewezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa nchi na wananchi kwa ujumla. Nassari pia amewatak...

OFISA MIPANGO ADAIWA KUBAKA

Picha
  Ofisa Mipango Miji katika Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi, Beno Mwenda (37) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 15. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 24, Kamanda wa Polisi mkoani humo Ally Makame amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo baada ya mama mzazi kumkabidhi mtoto huyo akiwa na mdogo wake ili awapeleka nyumbani kutoka baa walikokuwa wakinywa pombe. "Aliwapakiza kwenye gari lake alipofika njiani mtuhumiwa aliegesha gari pembeni ya barabara kisha kufanya unyama huo ndani ya gari lake," amesema Makame. Amesema baada ya tukio hilo kuripotiwa mtuhumiwa alikamatwa na upelelezi ulikamilika na kwamba amefikishwa mahakama ya Wilaya ya Mlele kujibu tuhuma zinazomkabili.

Simba Kutambulisha Kiungo Mkabaji Morice Chukwu

Picha
  MABOSI wa Simba SC, wamefikia makubaliano na kiungo mkabaji wa Rivers United, Morice Chukwu raia wa Nigeria, ambaye muda wowote atatambulishwa kikosini hapo kabla ya usajili kufungwa.   Kiungo huyo anatajwa kuwa ni pacha wa Nelson Okwa wakati wakiwa kwenye kikosi cha Rivers United, kabla ya Okwa hajajiunga na Simba hivi karibuni.   Simba chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Zoran Maki, imepanga kumtoa kwa mkopo kiungo mkabaji, Victor Akpan kurudi Coastal Union, ikiwa ni miezi michache tangu atambulishwe kikosini hapo.   Mpango wa Simba kumtoa Akpan ni kufuatia kiungo huyo kushindwa kuonesha kiwango bora mazoezini, hivyo Zoran akaomba aletewe kiungo mwingine mkabaji.   Taarifa za uhakika kutoka nchini Nigeria, zimebainisha kwamba, kila kitu juu ya usajili wa kiungo huyo kutua Simba kipo tayari. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Rivers United, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, suala la Chukwu kutua Simba limekamilika kwa asilimia kubwa, kinachosubiriwa kwa sasa ni mc...

ASKARI ALIYEMTESA MTUHUMIWA AKIWA KUFUNGWA PINGU AKAMATWA

Picha
  Jeshi la Polisi nchini Tanzania limeonya vitendo vya baadhi ya askari wake kuwapiga watuhumiwa na kusisitiza hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.  Hili limekuja kufuatia kusambaa kwa video mitandaoni inayomuonyesha askari akimpiga mtuhumiwa aliyeiba simu na kukiri kufanya tukio hilo na kuonyesha mtu aliyemuuzia simu hiyo. Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Agosti 23, 2022 na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza askari huyo tayari ameshachukuliwa hatua na sasa yupo mahabusu. Misime amesema kitendo hicho si tu kinyume cha sheria bali ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi hivyo hatua za kinidhamu dhidi ya askari huyo zitachukuliwa “Tukio hilo limeshachukua hatua kuanzia jana na kamanda wa Polisi Kinondoni, askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake,” amesema na kuongeza: “Jeshi la polisi litaendelea kusimamia nidhamu, haki, weledi na uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari anayekiuka sheria ...

WAOMBA WAPATIE BANGI ILI WAHESABIWE( SENSA)

Picha
  Wakati Serikali ikitoa nyamapori ya nyumbu 20 kwa jamii ya wawindaji, waokota matunda, wakusanya mizizi na warina asali ya wahadzabe wa bonde la Yaeda Chini Wilayani Mbulu Mkoani Manyara ili wahesabiwe, baadhi yao wamelalamika kunyimwa bangi katika mgawo huo.  Hii ni mara ya pili Wahadzabe hao kutaka wapatiwe nyama pori ili wahesabiwe kwani sensa iliyofanyika mwaka 2012 walitaka wapatiwe nyama ya nyani na bangi ili washiriki sensa ila wakapewa nyama na kunyimwa bangi. Akizungumza baada ya kupewa nyama hiyo leo Agosti 23, kazi wa mkazi wa Kijiji cha Mongoamono, Malam Dodokhoye amesema japokuwa atashiriki sensa ya watu na makazi na wenzake baada ya kupewa nyama hizo ila wamesikitishwa kunyimwa bangi. “Tunamshukuru mtoto wa Nyerere kwa kutupatia nyama ya nyumbu ila amekataa tusiletewe bangi, japokuwa tumekubali tutashiriki sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa huku Yaeda Chini,” amesema Dodokhoye.  Naye mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Abdi Soka amesema hadi saa tano asubu...

VIBAKA WAIBA VISHIKWAMBI VYA MAKARANI

Picha
  Wakati sense ya Watu na Makazi ikiendelea nchini, makarani wawili wamejikuta katika wakati mgumu baada kuporwa vifaa vyao vya kukusanyia taarifa maarufu kama vishikwambi na vibaka. Tukio la kwanza limetokea jijini Arusha ambapo karani aliyetambuliwa kwa jina la Saraphia Kiwango ameporwa kishikwambi chake alipokuwa akielekea kuanza kuhesabu makundi maalum katika Kata ya Unga Ltd jijini hapa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 23, Diwani wa Unga Ltd, Mahmoud Said amesema alipokea taarifa usiku wa kuamkia Agosti 23, kuwa kuna karani ameibiwa kishikwambi na mumewe kujeruhiwa kichwani na bodaboda hao wawili. "Jana usiku hawa makarani wa Sensa waliitwa kwa mtendaji wakati wanakwenda huko ndiyo wakakutana na vibaka waliokuwa kwenye bodaboda wakamjeruhi mumewe na kumpora kishikwambi kisha kutoweka kusikojulikana," amesema. Mtendaji wa Kata hiyo, Sophia Laizer amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa karani huyo baada ya kuibiwa kishkwambi hicho na kuwa alivamiwa na v...

SOMA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO

Picha