MAJAMBAZI YAMPORA MENEJA WA KITUO CHA MAFUTA ILEJE MAMILIONI AKIPELEKA BENKI

 


Majambazi yenye silaha yamemvamia Meneja wa Sheli ya Hike ilioko Isongole Wilayani  aliefahamika kwa Jina moja Matha wakati akipeleka fedha hizo benki iliopo Kata Itumba.



Mashuhuda wa tukio hilo wadai kuwa  Majambazi hayo yalijifanya kama wateja wa usafiri na kusimamisha bajaji aliokuwa kapanda Meneja huyo maeneo ya Isongole kitongoji cha Chumba geni B jirani na Daraja na Kisha kumtoa Meneja ndani ya Bajaji na kuanza kumporaji  na kutokomea na zaidi ya Milioni 30 walizopora kusikojulikana.


(MHE ANNA GIDARYA MKUU WA WILAYA ILEJE)

Mwenyekiti wa Usalama Wilayani Ileje ambae pia ndie Mkuu wa Wilaya Anna Gidarya amekiri kutokea kwa tukio hilo leo asubuhi na amesema atalizungumzia tukio hilo baadae kwani kwa sasa ameagiza Jeshi la Polisi na Vyombo vya Ulinzi vyote vya Ulinzi Ileje kufanya msako Mkali na tayari wameongeza nguvu ya vikosi vingine Wilayani humo ili waweze kuyakamata Majambazi hayo popote yalipo.



Tuachie Maoni yako hapo chini

Maoni

Unknown alisema…
Walijuaje kuwa meneja ana mzigo na kapanda hiyo bajaji?
Unknown alisema…
micholo ya hapohapo jambaz hawezi kuvizia mutu bira kumjua
Unknown alisema…
Uchunguzi uanzie kazini kwenu
Unknown alisema…
Waizi wako humo humo ndani ya sheli ni mchongo ulishapangwa
Unknown alisema…
Hapo walijuaje Kama bajaji mteja mojawapo ana hela na tunaomba huduma ya benki isogeee
Unknown alisema…
waliambiwa kuwa menej katok na mzigo
Unknown alisema…
Poleni Sana. Ktk kuelekea sikukuu ya Xmass matukio yaweza kuwa mengi tusipoweka na ulinzi imara

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA