MAJAMBAZI YAMPORA MENEJA WA KITUO CHA MAFUTA ILEJE MAMILIONI AKIPELEKA BENKI
Majambazi yenye silaha yamemvamia Meneja wa Sheli ya Hike ilioko Isongole Wilayani aliefahamika kwa Jina moja Matha wakati akipeleka fedha hizo benki iliopo Kata Itumba.
Mashuhuda wa tukio hilo wadai kuwa Majambazi hayo yalijifanya kama wateja wa usafiri na kusimamisha bajaji aliokuwa kapanda Meneja huyo maeneo ya Isongole kitongoji cha Chumba geni B jirani na Daraja na Kisha kumtoa Meneja ndani ya Bajaji na kuanza kumporaji na kutokomea na zaidi ya Milioni 30 walizopora kusikojulikana.
Mwenyekiti wa Usalama Wilayani Ileje ambae pia ndie Mkuu wa Wilaya Anna Gidarya amekiri kutokea kwa tukio hilo leo asubuhi na amesema atalizungumzia tukio hilo baadae kwani kwa sasa ameagiza Jeshi la Polisi na Vyombo vya Ulinzi vyote vya Ulinzi Ileje kufanya msako Mkali na tayari wameongeza nguvu ya vikosi vingine Wilayani humo ili waweze kuyakamata Majambazi hayo popote yalipo.
Tuachie Maoni yako hapo chini
Maoni